Sunday, November 15, 2015

UNYAMA !!!!! MWENYEKITI WA CHADEMA GEITA AUAWA

MWENYEKITI WA CHADEMA GEITA AUAWA
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Busanda, Alphonce Mawazo amefariki dunia kwa kupigwa na watu wasiojulikana leo saa 9 mchana, mkoani Geita.
Taarifa zinadai kuwa Mawazo ameuawa baada ya kutokea vurugu zilizohusisha wafuasi wa CHADEMA na CCM katika kata ya Ludete wakati wa harakati za kampeni kuelekea uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo uliopangwa kufanyika kesho Jumapili Novemba 15.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wakati vurugu hizo zikitokea, Alphonce alionekana kukimbizwa na kundi la watu lililokuwa likipiga kelele kuita watu wengine, na baadaye kundi hilo na watu wengine kumkamata na kuanza kumshambulia kwa kutumia zana mbalimbali ikiwemo mapanga na mawe kabla ya kufariki dunia akiwa hospitali kutokana na kuvuja damu nyingi

Unknown

1 comments:

  1. Christina:Playful exotic Mature Kenyan to satisfy all your needs come play with me all your fantasies come true doubles available.
    Nairobi Escorts
    Mombasa Escorts
    Kisumu Escorts

    ReplyDelete

 

Copyright @ 2013 HII NI LAANA.

Designed by Templateiy & CollegeTalks